1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Watu watatu wauawa katika maandamano jimbo la Kashmir

14 Mei 2024

Watu watatu wameuawa katika jimbo la Kashmir nchini Pakistan baada ya vikosi vya usalama kukabiliana na waandamanaji katika siku ya nne ya maandamano kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha.

https://p.dw.com/p/4fojy
Polisi wakirusha mabomu ya machozi wakati wa makabiliano na waandamanaji Muzaffarabad, Pakistani.
Polisi wakirusha mabomu ya machozi wakati wa makabiliano na waandamanaji Muzaffarabad, Pakistani.Picha: AMIRUDDIN MUGHAL/EPA

Afisa wa serikali na naibu kamishna wa Muzaffarabad, mji mkuu wa eneo hilo Nadeem Janjua amesema waandamanaji watatu wameuawa kwa kupigwa risasi na kwamba watu wengine wanane wamejeruhiwa.

Maelfu ya watu wameandamana tangu Ijumaa huku zaidi ya 10,000 wakijitokeza barabarani jana licha ya serikali kuahidi kutoa msaada wa kifedha katika jimbo hilo.

Soma pia: Chama cha Modi hakitasimamisha wagombea Kashmir

Serikali ilizima mtandao wa Intaneti na kutuma kikosi cha usalama kinachojulikana kama "Rangers" kukabiliana na waandamanaji.

Waziri Mkuu wa jimbo la Kashmir ameeleza kuwa afisa mmoja wa polisi pia aliuawawa katika ghasia za mwishoni mwa wiki na zaidi ya watu 100 walijeruhiwa.