1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ufaransa kujenga "ushirika sawa" na Afrika

Lilian Mtono
6 Aprili 2024

Ufaransa inalenga kurejesha uhusiano na Afrika na kujenga "ubia wenye uwiano" ambao utakua na manufaa kwa bara hilo.

https://p.dw.com/p/4eVEZ
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stéphane Séjourné
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stephane Sejourné yuko ziarani barani Afrika kuangazia namna ya kujenga uhusiano sawia na bara hiloPicha: SARAH MEYSSONNIER/AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Stephane Sejourné amesema hayo siku ya Jumamosi.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja Sejourné amemwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia Mudavadi kwamba, wito wa Ufaransa utakuwa ni kujenga upya ushirikiano sawia na wenye kuheshimiana na nchi za Afrika na kwa manufaa ya mataifa yote.

Sejourné aliyeteuliwa mwezi Januari ameanza ziara yake ya kwanza barani Afrika le Jumamosi nchini Kenya na baadaye ataelekea Rwanda kabla ya kuhitimisha nchini Ivory Coast.

Uhusiano kati ya Ufaransa na mataifa kadhaa ya Afrika yaliyowahi kuwa makoloni yake, umedorora huku bara hilo likizidi kuwa uwanja wa vita vya kidiplomasia, hasa ushawishi wa Urusi na China ukiongezeka