1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Kombora la Urusi latua karibu na msafara wa Zelensky

Sylvia Mwehozi
7 Machi 2024

Shambulio baya la kombora la Urusi katika mji wa bandari wa Odesa wa Ukraine, limeripotiwa kutua karibu na msafara wa Rais Volodymyr Zelensky na waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis.

https://p.dw.com/p/4dFIw
Volodymyr Zelensky na Kyriakos Mitsotakis.
Rais Volodymyr Zelensky na waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis mjini OdesaPicha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SERVICE/AFP

Shambulio baya la kombora la Urusi katika mji wa bandari wa Odesa wa Ukraine, limeripotiwa kutua karibu na msafara wa Rais Volodymyr Zelensky na waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis. Waziri mkuu wa Ugiriki aliyekuwa ziarani nchini Ukraine, amelielezea shambulizi hilo kuwa kubwa na la kushutukiza.

Mitsotakis amesema kuwa mwenyeji wake Zelensky alikuwa akimtembeza kwenye bandari ya Odesa, na kisha kusikia mlipuko mkubwa, muda mchache baada ya kuingia kwenye magari ya misafara.

Soma: Ukraine yadai kuharibu meli ya kivita ya Urusi kwenye Bahari Nyeusi

Jeshi la wanamaji la Ukraine limelieleza shirika la habari la AFP kwamba, shambulio hilo dhidi ya miundombinu ya bandari limewaua watu watano na wengine kujeruhiwa.

Urusi na Ukraine zimeongeza mashambulizi ya angani huku wanajeshi wa Moscow wakisonga mbele katika uwanja wa mapambano. Ukraine inakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi na silaha.