1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yathibitisha kufanya mazungumzo na Marekani nchini Oman

19 Mei 2024

Iran imethibitisha kwamba ilifanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani licha ya mataifa hayo mawili yaliyo mahasimu wakubwa kutokuwa na mahusiano rasmi ya kidiplomasia.

https://p.dw.com/p/4g34L
Bendera za Iran na Marekani
Kwa miongo kadhaa, Iran na Marekani zimekuwa mahasimu kutokana na tofauti za mitizamo na itikadi. Picha: Dado Ruvic/REUTERS

Siku ya Ijumaa tovuti ya masuala ya habari ya nchini Marekani Axios iliripoti kwamba maafisa wa Marekani na Iran walifanya mazungumzo hayo nchini Oman yakiwa na lengo la "kuepusha kutanuka kwa mashambulizi" kwenye kanda ya Mashariki ya Kati.

Taarifa hizo zimethibitishwa usiku wa kuamkia leo na shirika la habari la Iran, IRNA, likimnukuu afisa mmoja wa serikali ya Tehran. Afisa huyo ambaye ni mwakilishi wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa amesema mazungumzo hayo hayakuwa ya kwanza na wala hayatokuwa ya mwisho.

Yalifanyika siku chache baada ya Iran kuvurumisha makombora na droni kuelekea Israel mnamo Aprili 14 kujibu hujuma iliyofanywa na Israel kwenye ubalozi wake mdogo nchini Syria