1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Helikopta iliyombeba rais wa Iran yapata ajali

19 Mei 2024

Helikopta iliyombeba Rais Ebrahim Raisi wa Iran imepata ajali magharibi mwa nchi hiyo leo na vikosi vya uokoaji vimetumwa kuitafuta.

https://p.dw.com/p/4g3KW
Iran Raisi
Helikopta inayotumika kumsafirisha Rais Ebrahim Raisi wa Iran.Picha: vista.ir

Hayo yametangazwa na televisheni ya taifa ya Iran muda mfupi uliopita ikimnukuu waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Ahmed Vahidi.

Waziri huyo amesema hali mbaya ya hewa na ukungu mzito ndiyo chanzo cha ajali hiyo na kwamba huenda itachukua muda kwa vikosi vya waokoaji kulifikia eneo la mkasa huo.

Hadi sasa bado hakuna taarifa kuhusu hali ya rais Ebhahim ambaye alikuwa safarini pamoja na waziri wa mambo ya kigeni na gavana wa jimbo la Iran liitwalo Azerbaijan Mashariki.

Inaarifiwa ajali hiyo imetokea karibu na mji wa Jolfa ulio jirani na taifa la Azerbaijan na kiasi umbali wa kilometa 600 kutoka mji mkuu wa Iran, Tehran.

Rais Ebrahim alikuwa nchini Azerbaijan mapema hii leo kuzindua bwawa la kufua umeme akiwa pamoja na rais Ilham Aliyev wa nchi hiyo.