1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yaidhinisha makubaliano ya kudhibiti wahamiaji

Saumu Mwasimba
14 Mei 2024

Mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya yameidhinisha mageuzi kadhaa katika mfumo wake wa kupokea wahamiaji na waomba hifadhi wanaoingia Ulaya.

https://p.dw.com/p/4fqaX
Njia ya wakimbizi ya El Hierro
Wahamiaji wanawasili kwa mashua ndogo kwenye bandari ya La Restinga kwenye kisiwa cha El Hierro Februari 4, 2024.Picha: Europa Press/AP Photo/picture alliance

Hatua hiyo ni katika wakati ambapo kampeni za uchaguzi wa bunge la Ulaya utakaofanyika mwezi ujao, zimepamba moto. Suala la uhamiaji linatarajiwa kuchukuwa sehemu kubwa ya kampeini za uchaguzi huo. Makubaliano hayo mapya ya Uhamiaji  yameidhinishwa rasmi na mawaziri wa uchumi wa mataifa 27 wanachama na kumaliza zaidi ya miaka 8 ya mchakato wa kuyaandaa. Makubaliano hayo yatasimamia mfumo wa kuwashughulikia watu wanaoingia Ulaya kinyume cha sheria.Hungary na Poland ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikipinga utaratibu wa aina yoyote wa kulazimisha nchi kuwapokea wahamiaji au kutowa fedha kwaajili ya wahamiaji hao,zimepiga kura ya kuyapinga makubaliano hayo.